UKUAJI WA VIWANDA NCHINI WAPUNGUA… CHANZO?
Msukumo wa taifa la kenya wa kuwa na viwanda maarufu zaidi unarudishwa nyuma na miundombinu dhaifu na mapungufu ya ujuzi, kufuatia ripoti mpya ya bara la afrika.
Ripoti ya RED 2025 ya Maendeleo ya Viwanda barani Afrika na Baraza la Biashara la Afrika imetoa taarifa kwamba wakati Kenya ina nguvu katika ufadhili wa kidijitali na muunganisho, haina misingi muhimu inayohitajika kusaidia ukuaji wa viwanda.
Kenya ina alama nzuri katika viongeza kasi kama vile malipo ya kidijitali na uwazi wa kifedha. Hata hivyo, inafanya kazi vibaya katika viendeshi vya msingi vya viwanda kama vile nguvu za kutegemewa, mifumo ya usafiri, sayansi na elimu ya kiufundi, na ukuaji wa viwanda vikubwa vya ndani.
Vile vile ripoti hiyo inaonyesha Kenya inaafikia tu kiwango kimoja cha vichochezi saba kuu vya kuwa maarufu katika viwanda ambacho ni cha kidijitali—kinayoashiria kuegemea kupita kiasi kwa teknolojia bila usaidizi wa kutosha kutoka kwa viwanda vya jadi.Inaonya kuwa kukosekana kwa usawa huko kunaweza kusababisha ukuaji wa uchumi ambao hautoi nafasi za kutosha za kazi au kupanua utengenezaji.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































