#Local News

LUSAKA AWAHIMIZA VIJANA KUTUMIA MITANDAO KWA MAENDELEO

Vijana katika Kaunti ya Bungoma  wamehimizwa kutumia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali kama njia ya kujipatia kipato na kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumza katika eneo la Ndengelwa, Gavana Ken Lusaka amewataka vijana kuacha matumizi mabaya ya mitandao na badala yake kuitumia kwa manufaa yao binafsi.

Lusaka ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kidijitali katika eneo hilo, akisisitiza umuhimu wa teknolojia katika kuwainua vijana kiuchumi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *