SERIKALI KUIMARISHA MCHAKATO WA KUWAJIRI POLISI
Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema serikali itaanzisha hatua kali zaidi katika mchakato wa kuajiri maafisa wa polisi ili kuimarisha nidhamu na weledi ndani ya huduma ya kitaifa ya Polisi.
Hatua hiyo imefuatia kufukuzwa kwa makurutu 54 baada ya kubainika kuwa baadhi yao walikuwa na nyaraka za kughushi, hukumu za awali za uhalifu pamoja na visa vya ujauzito wakati wa mafunzo.
Kamanda wa chuo cha kitaifa cha Polisi Kiganjo Munga Nyale amethibitisha hatua hiyo wakati wa tathmini ya maendeleo ya mafunzo ya msingi ya makurutu hao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































