#Local News

FAMILIA YA JAMAA “ALIYERUSHWA’ YALILIA HAKI

Polisi wameimarisha uchunguzi katika tukio ambapo mwanamme mwenye umri wa miaka 25 alifariki baada ya kuripotiwa kurushwa nje ya basi la uchukuzi ambalo hatimaye lilimkanyaga hadi kufa kwenye barabara ya Kitengela kuelekea Namanga kaunti ya Kajiado Jumanne usiku.

Familia ya Joseph Mureithi imesema kwamba jamaa yao alikuwa akirejea nyumbani kutoka kazini aliporushwa nje ya basi hilo la kampuni moja maarufu, ambayo imesema inaendesha uchunguzi kwenye mazingira yaliyosababisha tukio hilo.

Tayari dereva na utingo wa basi hilo walikamatwa na maafisa wa DCI waliokuwa wakishika doria kwenye barabara hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *