#Local News

REJESHA EDUAFYA, SERIKALI YATAKIWA

Washikadau katika sekta ya elimu wameitaka serikali kurejesha mara moja mpango wa bima ya afya ya wanafunzi ya EduAfya, ili kudhibiti kile ambacho wametaja kama ongezeko la ghafla la vifo vinavyoweza kuzuiwa vya wanafunzi shuleni.

Kulingana na shirika la Elimu Bora, ongezeko la hivi punde la mikasa kwenye shule mbali mbali nchini limeweka wazi udhaifu mkubwa katika kukabiliana na hali za dharura, uangalizi na utekelezaji wa viwango vya usalama shuleni.

Wameshinikiza uchunguzi huru na wazi katika baadhi ya vifo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *