MASENETA WAKARIRI HAJA YA MAGAVANA KUAGIZWA
Huku mvutano ukiendelea kati ya maseneta na magavana kuhusu uwajibikaji wa matumizi ya fedha za umma, maseneta wamesisitiza umuhimu wa magavana kufika mbele ya bunge hilo kuweka wazi jinsi serikali zao9 zinavyowajibika mahitaji ya umma.
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, amekariri kuwa kuna maswali mengi kuhusu matumizi ya fedha za umma katika kaunti mbali mbali ikiwemo Nairobi, ambayo gavana Johnson Sakaja ametakiwa kujibu.
Ametetea ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali kuhusu matumizi hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































