GACHAGUA APIGA HATUA KUSHINIKIZA FIDIA
Kesi ya kushinikiza fidia kutokana na kutimuliwa kutoka afisini kwa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, itaendelea wiki ijayo baada ya kikao cha pili hapo jana ambapo Gachagua alifanikiwa kuishawishi mahakama kuidhinisha ushahidi kwamba aliugua ghafla hoja dhidi yake ilipokuwa ikijadiliwa katika bunge la seneti.
Licha ya pingamizi za mawakili wa serikali kuhusiana na ushahidi huo, mawakili wa Gachagua walisisitiza kwamba mteja wao alilazwa hospitalini na hivyo kukosa muda wa kujitetea seneti jinsi inavyotaka sheria.
Kwenye hatikiapo, imeibuka kwamba Rais William Ruto binafsi alimpigia simu daktari wa Gachagua kujua hali ya afya ya naibu huyo wake wa zamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































