#Local News

11 WAJERUHIWA RUMOS HILL WEST POKOT

Shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo la Rumos Hills kaunti ya West Pokot kufuatia mkasa wa kuporomoka kwa mgodi na kuwajeruhi watu 11 huku wengine kadhaa wakiwa bado wamekwama kwenye mgodi huo.

Kulingana na shirika la Kenya Red Cross, mansura watatu wako katika hali mahututi, na wanatibiwa katika hgospitali ya rufaa ya Kapenguria walikopelekwa haraka.

Imearifiwa kuwa wanajamii walikuwa wakijihusisha na uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi huo bila idhini ya mamlaka.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *