SHA YATIKISWA, TENA
Mamlaka ya afya ya jamii, SHA, kwa mara nyingine inakabiliwa na hatari ya kuvunjiliwa mbali kutokana na kesi iliyowasilishwa mahakamani ambapo mlalamishi anataka amri itolewe kuizuia mamlaka hiyo kukusanya fedha kutoka kwa wakenya.
Kwenye kesi hiyo, mkenya kwa jina Francis Awino, anapinga uhalali wa SHA, akitaka izuiwe kuhudumu kama kampuni nyingine za bima kwa misingi kwamba inakiuka sheria, ikiwemo madai kwamba SHA haijaweka wazi msingi wa sheria inayotumika kinyume na kifungu cha 35 cha katiba.
Jaji Bahati Mwamuye amemwagiza mlalamishi kuwasilisha nyaraka za kesi kwa wahusika kufikia leo huku kesi hiyo ikitarajiwa mahakmani tarehe 9 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































