#Local News

SERIKALI KUIMARISHA MCHAKATO WA KUWAJIRI POLISI

Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema serikali itaanzisha hatua kali zaidi katika mchakato wa kuajiri maafisa wa polisi ili kuimarisha nidhamu na weledi ndani ya huduma ya kitaifa ya Polisi.

Hatua hiyo imefuatia kufukuzwa kwa makurutu 54 baada ya kubainika kuwa baadhi yao walikuwa na nyaraka za kughushi, hukumu za awali za uhalifu pamoja na visa vya ujauzito wakati wa mafunzo.

Kamanda wa chuo cha kitaifa cha Polisi Kiganjo Munga Nyale amethibitisha hatua hiyo wakati wa tathmini ya maendeleo ya mafunzo ya msingi ya makurutu hao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *