KARUA AKOSOA KAULI ZA KAREN NYAMU KWA MWANAFUNZI
Shinikizo linaendelea kuongezeka dhidi ya Seneta mteule Karen Nyamu kufuatia matamshi yake yenye utata dhidi ya mwanafunzi wa Gredi ya Kumi wakati wa kikao cha Seneti.
Kiongozi wa People’s Liberation Party Martha Karua ameyataja matamshi hayo kuwa ya kusikitisha na yasiyokubalika, huku akiungana na viongozi wengine wanaotaka uwajibikaji kuhusu kauli hizo.
Karua amemtetea mwanafunzi huyo akisema Bunge linapaswa kuwa mahali pa kuwahamasisha vijana kuingia katika uongozi na utumishi wa umma badala ya kuwavunja moyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































