KCB YAPANIA KUKOMESHA UTAWALA WA KABRAS KENYA CUP
KCB RFC wanaamini wana uwezo wa kukomesha ubabe wa Kabras RFC watakapokutana katika fainali ya Kenya Cup msimu wa 2025/2026 katika uwanja wa ASK mjini Kakamega.
Hii itakuwa mara ya nane kwa timu hizo kukutana katika fainali tangu msimu wa 2014/2015, huku Kabras wakisaka taji lao la tano mfululizo katika mashindano hayo.
KCB wameingia fainali wakiwa na kikosi kilichochanganya vijana wenye nguvu na wachezaji wenye uzoefu, hali inayowapa matumaini ya kutoa ushindani mkali dhidi ya mabingwa hao watetezi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































