SINOMA YAONDOA ‘NOMA’ YA MAZINGIRA
Kampuni ya China kwa jina SINOMA ya kuunda vifaa vya kuweka paa za nyumba imefungua kiwanda kipya nchini ili kulipatia soko la taifa hili vifaa hivyo vya bei nafuu, ambavyo ni vya kudumu na ni salama kwa mazingira.
Akizungumza mjini Machakos kwenye ufunguzi wa kiwanda hicho, meneja mkuu wa Kampuni ya SINOMA Wu Shuang, amesema Kenya na China zina uhusiano wa karibu wa kirafiki, na kampuni yake itatengeneza vifaa vya bei nafuu na vyenye ubora ambavyo vitakidhi mahitaji ya wakenya.
Kwa upande wake Gavana wa Kaunti ya Machakos, Wavinya Ndeti, amesema kuwa anafurahi kuwa teknolojia inayotumika itabadilisha jinsi paa za nyumba zinavyowekwa nchini, na kwamba kiwanda hicho kitatoa fursa kwa vijana kujifunza jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































