WAHUDUMU MAGARI: NA BADO!

Wahudumu wa magari mjini Busia wametetea hatua ya kupandisha nauli maradufu kwa wasafiri kutoka mjini humo kuelekea miji mingine, wakisema nauli itaendelea kuongezeka kwa kipindi cha wiki mbizi zijazo kutokana na idadi kubwa ya wasafiri. Haya yanajiri huku wasafiri wakilalamikia kiwango cha juu cha nauli wanayotozwa licha ya hali ngumu ya uchumi. Uhaba wa magari […]

WANAFUNZI 10 HOSPITALINI KUFUATIA AJALI KIMENDE

Wakati uo huo, wanafunzi 10 wa shule ya Bishop Okoth wamepelekwa katika hospitali ya kimisheni ya Kijabe kwa matibabu baada ya basi lao kuanguka katika eneo la Kimende kaunti ndogo ya Naivasha. Imearifiwa kwamba basi hilo lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi 46, lilikosa mwelekeo na kutoka nje ya barabara kuu ya Nairobi- Nakuru kabla ya kuanguka. Walioshuhudia […]

WATU 6 WAFARIKI, WENGINE WAJERUHIWA LONDIANI

Watu 6 wameaga dunia huku wengine 46 kujeruhiwa baada ya kuhusika kwenye ajali iliyohusisha basi na trela katika eneo la Fort Ternan kwenye barabara ya Londiani kuelekea Muhoroni mapema leo. Kamanda wa polisi kaunti ya Kericho James Ng’etich, amesema basi liligonga trela kutoka upande wa nyuma, magari yote yalipokuwa yakielekea upande wa Kisumu. Waliojeruhiwa wanatibiwa […]

JUBILEE YAMTETEA UHURU DHIDI YA ODM

Chama cha Jubilee kimejitokeza kumtetea kinara wake ambaye pia ni rais mstaafu Uhuru Kenyatta dhidi ya mashambulizi ya kisiasa kuhusiana na jinsi kampeni za aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga zilishughulikiwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Kauli ya Jubilee imejiri kufuatia malumbano ya wazi kati ya katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna na mkurugenzi […]

NIGERIA WATINGA ROBO FAINALI AFCON

Super Eagles wa Nigeria walipaa juu kwa juu na kuingi robo fainali ya dimba la taifa bingwa barani Afrika AFCON 2025 baada ya kuwapepeta the Mambas wa Msumbiji kichapo cha mabao 4-0 nchin Morocco jana usiku. Mshambulizi wa Galatasaray Viktor Osimhen alifunga mara 2, Ademola Lookman na Akor Adams wakifunga moja kila mmoja na kuwapa […]

RATIBA YA KENYA CUP VOLLEYBALL YATOLEWA

Shirikisho la mchezo wa Voloboli KVF limethibitisha kwamba toleo la pili la ubingwa wa Kenya Cup Volleyball litaandaliwa kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 18 mwezi huu katika uga wa Kasarani Indoor Arena. Tangazo linaashiria mwanzo rasmi wa kalenda ya voliboli katika msimu wa 2025-26, ambapo timu za wanaume na wanawake zitashiriki. Aidha, shirikisho hilo limesema […]

BEATRICE CHEBET NJE YA UWANJA 2026

Mshindi wa nishani ya dhahabu 2 katika mbio za mita 10,000 na mita 5,000 katika mashindano ya Paris Olympics 2024 Beatrice Chebet atakuwa nje ya mashindano mwaka huu baada ya kuchukua likizo ya kujifungua. Haya ni kulingana na tangazo la ajenti wake, likimaanisha kwamba mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 hatatetea taji lake katika […]

MADURO ASISITIZA ANGALI RAIS WA VENEZUELA

Rais wa Venezuela aliyebanduliwa mamlakani na jeshi la Marekani Nicolas Maduro, amekana mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na mashtaka mengine alipofikishwa katika mahakama za New York. Maduro mwenye umri wa miaka 63, amesisitiza kwamba angali rais wa Venezuela licha ya kubanduliwa na kutekwa nyara Jumamosi iliyopita.  Mkewe rais huyo Cilia Flores, pia amekana […]

AMOLLO: HATUJAPANGA KUMTIMUA SIFUNA

Naibu mwenyekiti wa chama cha ODM Otiende Amollo ambaye pia ni mbunge wa Rarieda, amesisitiza kuwa hakuna mchakato wowote ulioanzishwa wa kumtimua katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna jinsi inavyodaiwa. Kauli ya Amollo inajiri baada ya kuibuka mgawanyiko baina ya Sifuna na kiongozi wa walio wachache bungeni Junet Mohammed, kuhusu mchango wa shilingi milioni […]

HOFU YA AJALI BARABARANI

Hofu imeibuka nchini kuhusu ajali za barabarani, zaidi ya watu 20 wakiaga dunia kwenye ajali hizo katika kipindi cha siku 5 za mwanzo wa mwaka huu pekee huku wito ukitolewa kwa madereva kuwa makini. Hii ni baada ya watu 9 kufariki kwenye ajali katika eneo la Naivasha hapo jana na wengine 55 kujeruhiwa, ajali ambayo […]