#Local News

KINDIKI ATETA KUHUSU USHAHIDI MPYA

Naibu Rais Kithure Kindiki, ameitaka mahakama kuu ya Milimani kuruhusu mawakili kumhoji Daktari wa masuala ya moyo, Dan Gikonyo, kuhusiana na ushahidi wake mpya ulioidhinishwa na mahakama hiyo katika kesi ya kubanduliwa kutoka afisini kwa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua.

Hatua ya Kindiki inajiri siku 3 tu baada ya mahakama hiyo kuidhinisha kutumiwa kwa ushahidi huo ambapo Dakta Gikonyo anasema Gachagua alilazwa hospitalini wakati hoja ya kumbanduliwa ikijadiliwa seneti, mawakili wakishikilia kuwa hatua hiyo ilimnyima Gachagua fursa ya kujitetea.

Hata hivyo, Kindiki anashikilia kuwa ushahidi huo unaweza tu kuthibitishwa kupitia mahojiano na mawakili.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *