#Football #Sports

FKF-WPL: BULLETS WAFYATUA TAJI, TENA

klabu ya Kenya Police Bullets ilijinyakulia taji la tatu la ligi kuu ya soka ya wanawake nchini, FKF-WPL kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Trinity Starlets hapo jana.

Kutokana na ubingwa huo, Bullets imekuwa klabu ya kwanza nchini kunyakua ubingwa mara 3 mfululizo katika misimu yake mitatu ya kwanza.

Bullets waliingia katika pambano hilo wakiwa kileleni na pointi 46, 2 mbele ya Ulinzi Starlets, ambao walikuwa wamecheza mechi moja zaidi.

Zikiwa zimesalia mechi 2 pekee kabla ya msimu kutamatika, Police walihitaji alama 3 tu kutawazwa mabingwa ikiwa imesalia mechi 1.

Kwa upande wao, Trinity waliingia mchezoni wakilenga kunyakua nafasi ya 3 na kuchelewesha azma ya Bullets kutawazwa mabingwa ila wakafeli, Margaret Kunihira akiwafungia mabingwa hao bao la pekee la mchezo kupitia mkwaju wa penalti.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *