AFRICA FORWARD SUMMIT KUKAMILIKA LEO
Kongamano la Africa Forward Summit lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Kenya na Ufaransa linakamilika hii leo baada ya kuanza rasmi hapo jana jijini Nairobi.
Kwenye majadiliano katika kongamano hilo la siku mbili, Rais William Ruto na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, wameeleza haja ya bara Ulaya kuwekeza katika bara la Afrika, ambalo wamelitaja kama linalokua kwa kasi.
Wamelitaka bara hilo kutoa kipaumbele kwa uwekezaji wa vijana, teknolojia, miundomsingi na elimu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































