#Local News

BEATRICE WANGARI AACHILIWA KUHUSIANA NA KIFO CHA OBWAKA

Mwanamke anayehusishwa na kifo cha mwenyekiti wa Bodi ya Nairobi hospital   Daktari Dr John Obwaka ameachiliwa huru huku uchunguzi kuhusu kifo hicho ukiendelea.

Jaji wa mahakama kuu Daiana Kavenza amemwachilia huru Beatrice Wangari kwa bondi ya binafsi ya shilingi laki moja baada ya mahakama kubaini kwamba hakuna ushaidi wa kutosha wa kuendelea kumzuilia zaidi.

Akitoa uwamuzi wake jaji Kavenza amesema hatua hii imechangiwa na matokeo ya upasuaji wa mwili wa marehemu uliofanyika Mei 5 na kuonyesha kuwa Daktari Obwaka alifariki kutokana na mshtuko wa moyo uliosababishwa na tatizo la moyo lililokuwa tayari linamsumbua.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *