DAKTARI GIKONYO AHOJIWA MAHAKAMANI KATIKA KESI YA GACHAGUA
Kesi ya kusikizwa kuondolewa Mamlakani aliyekuwa Naib Rais Rigadhi Gachagua inasikizwa Mahakamani
Daktari wa magonjwa ya moyo Daniel GiKonyo amedhibitisha kupokea simu kutoka kwa Rais William Ruto aliyetaka kujua hali ya kiafya ya aliyekuwa Naib Rais Rigadhi Gachagua baada ya kukimbizwa hospitalini wakati wa kusikizwa kwa hoja ya kumung’atua ofisini katika bunge la seneti.
Akizungumza katika mahakama Gikonyo amaeeleza kuwa ni jukumu lake kusema ukweli akikiri kumweleza Rais kuwa bado alikua anafanya vipimo,kulingana na Gikonyo baadae alimuomba Gachagua ruhusa ya kueka wazi kwa umma tatizo lililokuwa limemkumba wakati huo kabla ya kutotaarifu umma kuhusu hali ya afya yake.
Daktari Gikonyo amefika kuhojiwa kuhusiana na kiapo alichoapa kuhus ushaidi wake katika siku ya mwisho ya vikao hivyo kabla ya majaji wanaosikiza kesi hiyo kutangaza siku ambayo watatangaza uwamuzi wa kesi hiyo.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































