OMANYALA AJIANDAA KWA MBIO KALI SHANGHAI
Mwanariadha Ferdinand Omanyala anatarajiwa kushiriki mojawapo ya mbio ngumu zaidi msimu huu atakapowania mbio za mita 100 katika mashindano ya Diamond League Shanghai mwishoni mwa wiki hii.
Nyota huyo wa mbio fupi anaingia katika mashindano hayo akiwa katika kiwango kizuri baada ya kufanya vyema katika mashindano mbalimbali barani Afrika.
Omanyala alianza msimu wa mwaka 2026 kwa mashindano ya ndani kabla ya kushinda mbio zake za kwanza za mita 100 za nje mjini Stellenbosch kwa muda wa sekunde 10.19.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































