ODM YATANGAZA NAFASI ZA KUSAJILI WANACHAMA WA SIASA
Chama cha ODM kimefungua rasmi maombi ya uteuzi kwa wanasiasa wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 kupitia tiketi ya chama hicho.
ODM imewaalika wanachama kutoka kote nchini kuwasilisha maombi yao kabla ya tarehe 30 Juni mwaka huu.
Nafasi zilizotangazwa ni pamoja na Urais, ugavana, useneta, ubunge, uwakilishi wa wanawake pamoja na uwakilishi wadi kupitia njia ya mtamdao.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































