RAIS RUTO ATAJA NAFASI YA AFRIKA KATIKA MIFUMOYA KIAMATAIFA
Rais William Ruto ameendelea kusisitiza nafasi ya Afrika katika mifumo ya kimataifa pamoja na changamoto zinazokabili bara hili katika sekata ya Afya na maendeleo.
Akizungumza katika kongamano la Africa Forward Summit linaloendelea kwa siku ya pili jijini Nairobi, Rais Ruto amesema Afrika lazima ipate sauti sawa katika maamuzi ya kimataifa na kupunguza utegemezi wa misaada.
Aidha ameibua wasiwasi kuhusu kiwango cha uzalishaji wa dawa na change barani kutokana na changamoto zilizoshuhudiwa nchini wakati wa Covid 19.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































