#Local News

GHARAMA YA MITUMBA KUPANDA

Huenda Wakenya wanaotegemea biashara za nguo za mitumba wakalazimika kugharamika zaidi kuagiza nguo hizo kutokana na mpango wa serikali kurejesha ushuru wa bidhaa hizo kwenye mwaka wa kifedha wa 2026-27.

Kwenye mapendekezo katika mswada wa mwaka ujao wa kifedha, Waziri wa fedha John Mbadi amefafanua kuwa ushuru huo utafanyiwa marekebisho kabla ya kurejeshwa, akihoji kuwa lengo ni kurahisisha ukusanyaji ushuru katika sekta hiyo.

Hata hivyo, amekanusha kwamba serikali inalenga kuleta ushuru mpya kwa maji ya chupa na simu za mkononi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *