#Local News

UCHAGUZI MDOGO: WAKAZI EMURUA DIKIIR WAHAKIKISHIWA USALAMA

Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya chaguzi ndogo katika eneo bunge la Emurua Dikiir na wadi mbili katika kaunti za Samburu na Elgeyo Marakwet, mshirikishi wa eneo la bonde la ufa Abdi Hassan amewahakikishia wakazi wa Emurua Dikiir kwamba usalama wao umeimarishwa.

Katika kikao na wanahabari baada ya mkutano na maafisa wa usalama, amesema wanashirikiana na wadau wote wakiwemo maafisa wa tume ya IEBC ili kuhakikisha amani na usalama wakati na baada ya uchaguzi huo wa ubunge.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *