DEMBELE MCHEZAJI BORA UFARANSA
Mshambulizi wa Paris Saint-Germain Ousmane Dembele hapo jana alitajwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya soka nchini Ufaransa, Ligue 1, ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa bara Ulaya kunyakua Ligue 1 na kutinga fainali ya kombe la klabu bingwa bara Ulaya.
Dembele mwenye umri wa miaka 28, ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu kwa misimu miwili mtawalia, wa mwisho kufanya hivyo akiwa Zlatan Ibrahimovic mwaka wa 2014.
Amenyakua tuzo hiyo licha ya msimu wake kutatizwa na majeraha, akianzishwa katika mechi 9 pekee za Ligue 1, ikilinganishwa na mechi 20 alizoanzishwa msimu jana.
Klabu yake ya PSG ilinyakua taji la Ligue 1 Jumamosi kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brest, na kuwaacha pointi 6 kileleni mbele ya washindani wao wa karibu Lens.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































