#Football

SADIKI AWAVUTIA CHELSEA NA MANCHESTER UNITED

Kiungo wa Sunderland Noah Sadiki anadaiwa kuvutia vilabu vya Chelsea na Manchester United baada ya msimu mzuri wa kwanza nchini Uingereza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amesema mambo yamebadilika kwa haraka tangu aondoke Union SG, lakini hakutaka kufunga mlango kuhusu uwezekano wa kufanya uhamisho mkubwa katika dirisha la kiangazi.

Sadiki amesema kwa sasa anaangazia kumaliza msimu vizuri pamoja na kuiwakilisha DR Congo katika mashindano ya Kombe la Dunia.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *