#Football #Sports

AKONNOR AWATAKA WACHEZAJI KUMAKINIKA HISTORIA IKIBISHA

Klabu ya Gor Mahia itahitaji ushindi mara 3 pekee katika mechi zake 3 zilizosalia ili kutawazwa mabingwa mara ya 22 katika ligi kuu ya soka nchini, KPL, wakiwa mbele ya wapinzani wao AFC Leopards na pointi 7.

Safari ya kuelekea ubingwa huo ilitiwa miiba na sare ya bao 1-1 dhidi ya Police FC wikendi, Gor wakilazimika kutoka nyuma na kulazimisha sare hiyo baada ya awali Ingwe kuandikisha ushindi na kupunguza mwanya wa pointi.

Hata hivyo, licha ya sare hiyo, kocha mkuu Charles Akonnor amesalia na matumaini kwamba kikosi chake kitabeba taji hilo msimu huu, huku akiwataka wachezaji wake kumakinika zaidi mbele ya lango.

Amewahakikishia wafuasi wa K’Ogalo kwamba timu hiyo inacheza mchezo mzuri na kwamba hawafai kuwa na hofu kuhusu kutawazwa mabingwa.

Gor wamecheza mechi moja zaidi ya Ingwe, ambao iwapo watashinda mechi yao ya mkononi dhidi ya Ulinzi Stars, watapunguza pengo la pointi hadi 4 na kuwapa Gor shinikizo kuelekea utepeni.

Hata hivyo, Akonnor amesisitiza kwamba vijana wake watastahimili shinikizo zilizopo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

AKONNOR AWATAKA WACHEZAJI KUMAKINIKA HISTORIA IKIBISHA

GHARAMA YA MITUMBA KUPANDA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *