HALI TETE YA USALAMA BUNGOMA, BUSIA
Polisi katika kaunti za Busia na Bungoma wanachunguza matukio mawili yaliyohusisha mauaji ya mvulana mwenye umri wa miaka 12 na afisa wa afya aliyeuawa nyumbani kwake katika eneo la Nambaya, viungani mwa mji wa Bungoma.
Katika tukio la kwanza, polisi wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 33 kuhusiana na mauaji ya mwanawe katika eneo la Teso North aliyeripotiwa kupigwa, polisi wakisema shauku iliibuka wakati mwanamke huyo na mumewe walizuru afisi ya chifu kutaka kibali cha kumzika mwanao ila maelezo kuhusu kifo chake yakatofautiana.
Katika tukio la pili, afisa huyo wa afya kwa jina Pascal Wakafuta mwenye umri wa miaka 38, aliuawa nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana, washukiwa wakiaminika kujificha nyumbani kwake kabla ya kutekeleza mauaji.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































