#Football #Sports

OGOLLA ASIKITISHWA NA MIGOGORO NDANI YA FKF

Aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Kenya na kocha wa soka John Bobby Ogolla ameonyesha masikitiko yake kuhusu migogoro inayoendelea ndani ya FKF.

Shirikisho hilo limekumbwa na mivutano ya uongozi kati ya Rais Hussein Mohamed, naibu wake MacDonald Mariga pamoja na wanachama wengine wa kamati kuu, huku madai ya ubadhirifu wa fedha za bima ya mashindano ya CHAN yakitajwa kuchochea mvutano huo.

Ogolla amehoji ukosefu wa umoja miongoni mwa viongozi wa soka nchini akisema hali hiyo inaendelea kudhoofisha maendeleo ya mchezo wa kandanda Kenya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *