OPARANYA APONGEZA WAKENYA KWA KULIPA HUSTLER FUND
Waziri wa vyama vya ushirika Wycliffe Oparanya anasema kiwango cha ulipaji wa mkopo wa hustler fund kimeimarika pakubwa na kufikia asilimia tisini.
Akijibu maswali ya maseneta katika bunge la seneti hii leo, Oparanya amekiri kwamba kiwango cha kutolipa mkopo huo kilikuwa juu pindi ulipozinduliwa japo anakariri kwamba kila mkenya aliyekopa pesa hizo ataandamwa ili alipe.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































