#Football #Sports

JUNIOR STARLETS KAMBINI KABLA YA KUVAANA NA UGANDA

Mshambuliaji wa Junior Starlets, Faith Boke, amesema kikosi hicho kina imani ya kuichapa Uganda katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 17.

Kenya watavaana na Uganda katika mechi ya kwanza Mei 22 katika uwanja wa FUFA Stadium kabla ya marudiano kuchezwa Mei 30 katika Nyayo National Stadium. Starlets walifika hatua hiyo baada ya kuitoa Namibia kwa jumla ya mabao 7-1.

Akizungumza kambini Kasarani, Boke amesema wachezaji wameongeza makali mazoezini chini ya benchi la ufundi na wako tayari kuwakabili Uganda huku wakisaka kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *