BEI YA PETROLI, DIZELI YAVUKA SH.200
Wakenya kwa mara nyingine watalazimika kugharamika zaidi kwa mahitaji ya kila siku baada ya serikali kuongeza bei ya mafuta ya petroli kwa shilingi 16.65 kwa kila lita huku dizeli ikiongezeka kwa shilingi 46.29 kwa kila lita, bei hizo mpya zikitekelezwa kwa kipindi cha siku 30 zijazo.
Kwa mujibu wa mamlaka ya kudhibiti kawi na petroli nchini, EPRA, lita moja ya petroli jijini Nairobi itauzwa kwa shilingi 214.25, dizeli ikiuzwa kwa shilingi 242.92 hku lita ya mafuta taa ikisalia shilingi 152.78.
EPRA imesema ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa bidhaa za petroli katika soko la kimataifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































