#Local News

TIFA SURVEY: RUTO AONGOZA MBIO ZA URAIS NA 24%

Rais William Ruto anaongoza katika mbio za urais kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kulingana na utafiti uliofanywa na kampuni ya TIFA.

Kulingana na utafiti huo, Ruto anaongoza kwa asilimia 24 ya uungwaji mkono akifuatwa na Kalonzo Musyoka aliye na asilimia 19 kisha Fred Matiangi akiwa na asilimia 14.

Wengine ni pamoja na seneta wa Nairobi Edwin Sifuna akiwa na asilimia 10, Rigathi Gachagua na asilimia 9, Wagombea wengine wakiwa na asilimia 3 huku asilimia 15 ya waliohojiwa wakiwa hawajafanya uamuzi.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *