SING’OEI ATETEA UTOAJI WA PASPOTI KWA RSF
Wizara ya masuala ya kigeni imetetea kujihusisha kwa serikali katika juhudi za upatanishi nchini Sudan huku ikiendelea kukabiliwa na madai ya utoaji wa paspoti za usafiri kwa baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu wa kundi la wapiganaji la RSF.
Kwenye mahojiano na shirika moja la habari, katibu mkuu katika wizara hiyo Korir Sing’oei, amesisitiza kuwa Kenya inaendelea kujitolea kuunga mkono juhudi za kurejesha amani nchini humo kupitia mwongozo wa shirika la maendeleo la kikanda IGAD.
Amesema utoaji wa paspoti ulifanywa kwa misingi ya kibinadamu ili kuwasaidia wanaokimbia mapigano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































