UDA, DCP KUTOANA KIVUMBI EMURUA DIKIIR
Wakazi katika eneo bunge la Emurua Dikiir wameendelea kujitokeza kushiriki uchaguzi mdogo wa kumchagua mbunge wao kumrithi marehemu Johanna Ng’eno aliyewaongoza tangu mwaka 2013 eneo bunge hilo lilipobuniwa.
Zoezi la upigaji kura limeanza mapema leo, huku wapiga kura wapatao 44,000 wakitarajiwa kushiriki zoezi hilo linalowaniwa na wagombeaji watano, kivumbi kikali kikiwa baina ya UDA na DCP.
Tume ya IEBC imewahimiza wakazi kudumisha amani wanapojitokeza kupiga kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































