#Local News

WIZARA YA ELIMU YALALAMIKIA MGAO FINYU

Serikali imekiri uwezekano wa kutatizika kwa utoaji wa huduma za elimu ya kiufundi nae elimu ya juu nchini kutokana na uhaba wa fedha, ikisema shilingi bilioni 19 zinahitaji ili kufadhili utoaji wa elimu hiyo.

Akiwa mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu elimu, katibu mkuu katika idara ya masomo ya TVET, Daktari Esther Mworia, ameonya kuwa ukosefu wa fedha hizo unaweza kuongeza madeni ambayo hayajalipwa kwa wasambazaji wa huduma kwa taasisi hizo, mbali na wengi wa wanafunzi kukatiza masomo yao.

Idara ya sayansi, ubunifu na utafiri vile vile imelalamikia kupunguzwa kwa mgao wake kufuatia kuondolewa kwa shilingi bilioni 1.13 zilizokuwa zimetengewa maendeleo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *