#Local News

WAZEE WA VIJIJI KUPATA TABASAMU

Serikali imetangaza pendekezo la kuwalipa mshahara wa shilingi 3,000 kila mwezi wazee wa vijiji kote nchini, ambao ni takribani 110,000 kama njia mojawapo ya kutambua mchango wao katika mfumo wa utawala nchini.

Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu utawala na usalama, katibu mkuu katika wizara ya masuala ya ndani Raymond Omollo, amesema wazee walio chini ya mipango mingine ya serikali kama vile Inua Jamii na wahudumu wa afya ya nyanjani hawatapokea mshahara huo, akisema tayari sera imeandaliwa kufanikisha kuwatambua wazee wa vijiji.

Hata hivyo, kamati hiyo imependekeza mshahara wa shilingi 5,000 mbali na kuwekwa kwa mfumo rasmi wa sheria ili kufanikisha pendekezo hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *