#Football #Sports

ULINZI STARS WAPIGANIA NAFASI KUBAKI KPL

Kocha mkuu wa Ulinzi Stars, Mulinge Ndeto, amewataka wachezaji wake kucheza kwa ari ya ushambuliaji huku wakisaka kusalia katika Ligi Kuu ya Kenya. Ndeto amesema mechi tatu zilizobaki ni kama fainali kwa timu hiyo.

Ulinzi walipoteza mabao 2-0 dhidi ya AFC Leopards katika uwanja wa Nyayo National Stadium na kubaki nafasi ya 16 wakiwa na alama 32, alama moja nyuma ya Kariobangi Sharks huku zikiwa zimesalia mechi tatu kumaliza msimu.

Hata hivyo, Ndeto anaamini Ulinzi wana uwezo wa kujinasua na kuendelea kusalia katika ligi kuu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *