MUYOTI AIPA POLICE IMANI DHIDI YA BANDARI
Kocha mkuu wa Kenya Police FC, Nicholas Muyoti, amesema ana imani kikosi chake kitaibuka na ushindi watakapovaana na Bandari FC katika nusu fainali ya kombe la Mozzart Bet siku ya Jumamosi.
Muyoti amewataka wachezaji wake kubaki makini, wenye nidhamu na kudhibiti presha ya mchezo huo utakaochezwa katika Nyayo National Stadium.
Mshindi wa mashindano hayo atawakilisha Kenya katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































