#Football #Sports

ARTETA ASISITIZA MIFEREJI YA MABAO KULENGA UBINGWA

Kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta, amewataka vijana wake kuwabebesha Burnley mzigo wa mabao watakapokutana Jumatatu kwenye mechi yao ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza EPL, wanapolenga ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 22 iliyopita.

The Gunners wako mbele ya Manchester City na pointi 2 zikiwa zimesalia mechi mbili kabla ya kutamatika kwa ligi wikendi ijayo, ushindi wao wa mwisho ukijiri kufuatia utata wa VAR uliowapokonya West Ham United bao la kusawazisha katika dakika za mwisho ambalo huenda lingebadili mwelekeo wa ligi hiyo.

Hata hivyo, City wako mbele ya Arsenal na ubora wa bao 1, na watanyakua taji hilo iwapo watashinda mechi zao zote nao Arsenal wateleze dhidi ya Burnley au ugenini dhidi ya Crystal Palace kwenye mechi yao ya mwisho.

City yake Pep Guardiola, inaonekana kuwa na mechi ngumu ikiwemo safari ya Vitality Stadium dhidi ya Bournemouth ambao bado wanawania nafasi ya kushiriki ligi ya klabu bingwa bara Ulaya msimu ujao, na mechi ya mwisho nyumbani dhidi ya Aston Villa.

Arsenal watakosa huduma za beki wao Ben White ambaye atakuwa nje kwa kipindi kilichosalia cha msimu kutokana na jeraha alilovuna dhidi ya West Ham United.

Mwingine ni beki wa kulia Jurien Timber, ambaye pia huenda asicheze mechi ya EPL msimu huu, ingaa Arteta ana matumaini kwamba beki huyo atapona na kuejea kwenye fainali ya klabu bingwa dhidi ya PSG.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *