BEI MPYA YA MAFUTA KUTANGAZWA LEO
Wakenya wakisubiri bei mpya ya mafuta kutangazwa hii leo,serikali imetoa shilingi bilioni sita kwa wauzaji wa mafuta kufidia udhibiti wa bei za bidhaa hizo za mwezi uliopita kabla ya kutangazwa kwa makadirio ya bei za mafuta leo hii .
Kulingana na wauzaji bei ya petroli huenda ikapanda iwapo gharama zilizobebwa na waagizaji wa mafuta zitazingatiwa iwapo serikali haitaingilia kati kutoa ruzuku nyingine ya kuwakinga watumiaji dhidi ya ongezeko hilo.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































