#Rugby #Sports

KCB RFC WAELEKEZA DIRA 7S CIRCUIT BAADA YA KURAMBISHWA SUKARI

Kocha mkuu wa klabu ya raga KCB RFC Andrew Amonde, amewahimiza vijana wake kuzika masaibu ya kupoteza kwenye fainali za Kenya Cup siku ya Jumamosi na badala yake kuganga kutetea taji la National Sevens Circuit.

KCB ilijinyakulia taji hilo kufuatia ushindi wa 15-14 dhidi ya Strathmore wakati wa fainali ya 2025 Dala Sevens.

Hata hivyo, matayarisho ya kutetea taji hilo yanajiri huku klabu hiyo ikiuguza kichapo cha 14-8 kwenye fainali ya Kenya Cup iliyoandaliwa katika uwanja wa ASK Kakamega Showground, KCB wakianza kwa mkosi baada ya Festus Shiasi kuonyeshwa kadi nyekundu na kuwaacha wakiwa wachache uwanjani.

Ubingwa wa Kabras ni wa kihistoria, ukiwa wa 5 mfulullizo huku wakiongeza rekodi ya kutopoteza mechi hadi mechi 54 kuanzia mwaka wa 2022.

Kocha Amonde alikiri kwamba uzoefu ulikuwa nguzo kwenye fainali hiyo, ambao vijana wake walikosa.

Hata hivyo, anaamini kuwa kikosi chake kina nafasi ya kutetea ubingwa wa National Sevens Circuit.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *