#Local News

MUSEVENI KUAPISHWA LEO KUENDELEA KUHUDUMU

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ameratibiwa kuapishwa hii leo kuanza muhula wa saba madarakani, baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa hivi punde mapema mwaka huu.

Viongozi wa mataifa mbali mbali ya Afrika na kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo, akiwemo Rais William Ruto, Samia Hassan wa Tanzania, Felix Tshisekedi wa DRC, Salva Kiir wa South Sudan, Paul Kagame wa Rwanda, Emason Mnangagwa wa Zimbabwe miongoni mwa wengine.

Museveni ambaye ameongoza Uganda tangu mwaka wa 1986, ni miongoni mwa marais waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MUSEVENI KUAPISHWA LEO KUENDELEA KUHUDUMU

AYUB SAVULA AMSUTA GACHAGUA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *