SPURS WASALIA MATATANI NA SARE YA LEEDS
Mathys Tel aliwapandisha Tottenham na kuwazika tena katika eneo la kushushwa daraja baada ya kuwafungia bao na kisha kusababisha penalti iliyowaacha na sare ya bao 1-1 dhidi ya Leeds jana usiku.
Matokeo hayo yaliwaacha Spurs katika nafasi ya 17, pointi 2 juu ya West Ham walio katika nafasi ya 18 na kuacha hai kinyang’anyiro cha kushushwa daraja mwishoni mwa msimu.
Kwa sasa Tottenham watahitaji kujikaza katika mechi zao 2 zilizosalia na kuomba kwamba West Ham waendelee kuteleza ili kusalia kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Tel aliwapa vijana wa Roberto De Zerbi matumaini katika kipindi cha pili alipowaweka kifua mbele, ila Mfaransa huyo akacheza visivyo na kuwaacha Spurs katika hali ya hatari tena.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































