#Athletics #Sports

OKETCH KUCHUANA NA NASER ANAPOONJA DIAMOND LEAGUE

Mshikilizi wa rekodi ya kitaifa katika mbio za mita 400 Mercy Oketch, anajiandaa kwa kinyang’anyiro cha kupimana nguvu kwa mara ya kwanza katika mbio za Diamond League Jumamosi hii jijini Shanghai, Uchina.

Akiwa anashiriki kwa mara ya kwanza kwenye mbio hizo, Oketch atapambana na wanariadha wenye kasi zaidi ulimwenguni, akiwemo bingwa mara tatu wa fainali za mbio hizo Salwa Eid Naser wa Bahrain.

Oketch ameibuka kama chipukizi mwenye uwezo mkubwa wa kuangusha majabali katika majukwaa ya kitaifa na kimataifa katika mbio za mita 400, akishikilia nafasi ya 15 ulimwenguni.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23 ataingia katika mbio za Shanghai Diamond League akiwa na maruerue ya World Relays jijini Gaborone, ambako alimaliza wa nne kwenye kikosi kilichowajumuisha Mercy Chebet, George Mutinda na Kelvin Tonui.

Marekani iliibuka na ubingwa katika mashindano hayo huku Uingereza ikimaliza ya pili.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *