MWANIAJI WA UDA AIBUKA MSHINDI EMURUA DIKIRR
Mgombeaji wa ubunge katika eneo bunge la Emurua Dikirr kupitia tiketi ya chama tawala cha UDA David Keter, ametangazwa mshindi wa kiti hicho kwenye uchaguzi mdogo ulioandaliwa hapo jana, baada ya kujizolea jumla ya kura 18,266.
Kulingana na tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, mgombeaji wa DCP Vincent Rotich alimaliza wa pili akiwa na kura 10,760 baada ya kura za vituo vyote 94 kujumlishwa, IEBC ikisema jumla ya kura zilizohesabiwa ni 29,358.
Wawaniaji wengine 3 walipata chini ya kura 200 kila mmoja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































