#Football #Sports

AFCON U17: SA WAPAMBANIA USHINDI, TZ YASHINDA ANGOLA IKISHIKILIA MALI

Timu ya taifa ya Afrika Kusini ilitoka nyuma na kuandikisha ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal katika mechi yao ya ufunguzi kwenye dimba la mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17, AFCON U17.

Mashindano hayo yaliyoanza Jumatano wiki hii, yataendelea hadi mwanzoni mwa mwezi ujao nchini Morocco.

Senegal walitishia kuwatia donda Amajimbos baada ya kuchukua uongozi katika dakika ya 44 kupitia kwa Cheickh Thior, ila Afrika Kusini wakajizatiti na kufunga mabao hayo katika kipindi cha pili.

Inganathi Simama aliwarejesha Amajimbos mchezoni dakika ya 48 kabla ya kizaazaa katika eneo la hatari la Mali kusababisha Thior kujifunga bao chini ya shinikizo.

Katika matokeo mengine, mabao ya Dismas Athanasi, Razaki Mbegelendi na bao la kujifunga la Pascoal Miambo yaliwapa Tanzania ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Msumbiji.

Wakati uo huo, Angola walionyesha nidhamu na mchezo wa hali ya juu na kutka sare tasa dhidi ya Mali katika mechi yao ya Group C kwenye mashindano hayo.

Algeria na Ghana pia waliishia kwenye sare ya mabao 2-2

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

AFCON U17: SA WAPAMBANIA USHINDI, TZ YASHINDA ANGOLA IKISHIKILIA MALI

KIVUMBI CHA FKF CUP

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *