KESI DHIDI YA OKOTH OBADO YATUPILIWA MBALI
Aliyekuwa gavana wa Migori Okoth Obado watoto wake wanne pamoja na washirika wao wameondolewa mashtaka ya ufisadi wa shilingi milioni 73.5 baada ya mahakama ya kukabiliana na ufisadi ya milimani kuruhusu ombi la mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma la kuondoa kesi hiyo kufuatia makubaliano ya nje ya mahakama.
Katika uamuzi wake hakimu Celisa Okore amesema mahakama imeridhika kwamba ODPP hakutumia vibaya mamlaka yake katika kufanikisha makubaliano hayo na kuyapitisha rasmi kama hukumu ya mahakama.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































