OPIYO WANDAYI AELEZA SABABU ZA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA
Waziri wa Kawi na Petroli Opiyo Wandayi amesema ongezeko la bei ya mafuta nchini limechangiwa na hali ya soko la kimataifa kufuatia mvutano unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati huku akiwahakikishia Wakenya kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta na hakuna uhaba unaotarajiwa kwa sasa.
Wandayi amesema serikali ina mpango wa kuhakikisha mafuta yanaingia nchini bila changamoto na kuongeza kuwa shehena nyingine za mafuta tayari ziko njiani kuingia nchini ili kuimarisha usambazaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa wananchi pamoja na sekta mbalimbali za uchumi.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































