#Local News

OPIYO WANDAYI AELEZA SABABU ZA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA

Waziri wa Kawi na Petroli Opiyo Wandayi amesema ongezeko la bei ya mafuta nchini limechangiwa na hali ya soko la kimataifa kufuatia mvutano unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati huku akiwahakikishia Wakenya kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta na hakuna uhaba unaotarajiwa kwa sasa.

Wandayi amesema serikali ina  mpango   wa kuhakikisha mafuta yanaingia nchini bila changamoto na kuongeza kuwa shehena nyingine za mafuta tayari ziko njiani kuingia nchini ili kuimarisha usambazaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa wananchi pamoja na sekta mbalimbali za uchumi.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *